RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA MAREHEMU SAJUKI....
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 9:49 PMYULE MWANAJESHI ALIYEPIGA PICHA NA GODBLESS LEMA AKAMATWA NA KUTIWA NGUVUNI
Posted by Bigie habari za kitaifa 9:40 PM Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari, ila aliwahi kuwa JKT na akaacha.
Amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa Mererani wanamtambua kama mwanajeshi.
PICHA ZA UTUPU ZAENDELEA KUUTAFUNA UTAMADUNI WETU.....
Posted by Bigie habari za kitaifa, picha za utupu 9:34 PMTamaa ya pesa imeendelea kuwa kikwazo katika maisha yetu ya kila siku.......
Matuko ya ajabu yenye tamaduni za nchi za magharibi yameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika mila na tamaduni zetu.....
Huyu ni binti aliyefahamika kwa jina moja la Jackline.Yeye na bahasha wake inaonesha hawazitambui thamani na utu wa mwafrika.....
HUU NI WAKATI MWAFAKA WA SERIKALI ZETU KUCHUKUA HATUA STAHIKI.....
ASANTE MDAU KWA PICHA
MWILI WA SAJUKI WAHAMISHIWA MSIKITINI HUKU MAANDALIZI YA MAZISHI YAKIENDELEA
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 1:55 PMMWILI msanii nyota wa filamu, Juma Kilowoko “Sajuki” aliyefariki juzi alfajiri, umeondolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospital ya Taifa, Muhimbili.
Na badala yake, mwili wa Sajuki sasa umekwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha msikiti wa Shadhir (Masjid Shadhully) uliopo Kariakoo mtaa wa Sikukuu na Twiga.
Msanii Issa Mussa “Cloud” aliiambia mpekuzi kuwa lengo la kuhamisha mwili huo ni kujaribu kufanikisha taratibu zote za kesho kwenda na muda.
“Muhimbili process za kuchukua mwili ni ndefu na hata huduma zao za kuosha mwili wa marehemu ni ndefu pia kutokana na wingi wa maiti zinahofadhiwa na kuoshwa hospitalini hapo.
“Hivyo tumeona tuupeleke mwili Masjid Shadhully kwa vile hakuna msongamano kama wa Muhimbili” alisema Cloud.
Masjid Shadhully ndio msikiti atakaoswaliwa Sajuki ambapo mwili wake utachukuliwa msikitini hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa nyumbani kwake Tabata na baadae kurudishwa tena Masjid Shadhully kwa ajili ya kuswaliwa na kwenda kuzikwa makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Ijumaa saa 7 za mchana.
MAANDALIZI YA MSIBA

Wasanii wa filamu Mike Sangu (kushoto) Jacob Steven ‘JB’ (katikati) na Denes Sweya ‘Dino’ wakipanga mikakati msibani hapo.

Mke wa marehemu Sajuki, Wastara Juma ‘Stara’, aliyejifunika akifarijiwa na waombolezaji.

JB akimpa pole mama yake mzazi Sajuki

Stara akiwa katika maombolezo.

JBakijiweka tayari kwa shughuli za msibani.

Baba wa marehemu Sajuki, mzee Kilowoko, akimsikiliza JB.
MAANDALIZI ya kumzika msanii wa filamu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ yanaendelea nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.
Habari za kuaminika ni kwamba Sajuki atazikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo saa mchana.
JOSEPH MBILINYI ( MBUNGE WA MBEYA) IJUMAA ATAKUWA MGENI RASIMI KATIKA UFUNGUZI WA INTERNET CAFE YA IZZO B
Posted by Bigie habari za kitaifa, sugu 1:07 PMMbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa internet cafe ya rapper Emmanuel ‘Izzo B’ Simwinga.
Ofisi hiyo iitwayo Izzo Bizness Internet Cafe & Secretarial Bureau ipo TEKU University jijini Mbeya.
Akiongea na mtandao huu , Izzo amesema katika uzinduzi huo utakaoanza saa 8 mchana hakutakuwa na performance yoyote bali watafungua champagne za kutosha.
"Kesho mungu akisaidia ntafanya ufunguzi rasmi wa Internet cafe yangu iliyopo MBEYA chuo Cha Teofilo kisanji(TEKU) NA Mgeni rasmi atakuwa MH:Joseph mbilinyi mbunge wa mbeya...
Kama uko MBEYA na unataka kushuhudia uzinduzi wa ufunguzi wa Internet cafe yangu iliyopo chuo Cha teku MBEYA utakaofanywa na Mh: Joseph Mbilinyi mbunge wa MBEYA Mjini unaweza kuja hakuna kiingilio muda ni saa Nane Mchana...karibuni".....Izzo b
"NILISHAURIWA NA MAMA YANGU KURUDI MACHOZI BAND"....MWINYI
Posted by Bigie ABDALLAH MWINYI, BONGO FLEVA, habari za kitaifa 9:39 AMKama unakumbuka siku zilizopita Lady Jaydee aliweka ujumbe katika ukurasa wa facebook na kuomba maoni kutoka kwa wananchi kuhusiana na Mwinyi,kurudi katika band yake,sasa leo Mwinyi ameeleza ukweli na kusema kwamba hakuwa na ndoto za kurudi katika band hiyo bali ni mama yake mzazi ndiye alimshauri na ndiyo maana ameweza kurudi tena kundini.
Hayo ndiyo maneno ya Mwinyi baada ya kuamua kuweka ukweli juu ya Machozi Band.
HAYA NDO MANENO MAZITO YA MWISHO ALIYOYASEMA MAREHEMU SAJUKI KUHUSU WASTARA
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 3:29 AMAmeongea AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.
Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.
Masanja Mkandamizaji na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.
Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”
Mbali na hayo, Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”
JIHADHARI NA WEZI WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MSIBA WA SAJUKI
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 2:52 AMKwa mujibu wa Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia jana, kumejitokeza watu wanaojifanya kutumwa na familia kuchangisha fedha kwa njia ya simu.
Steve amesema kuna mtu mmoja anayetumia jina kubuni Tumaini ameendelea kukusanya fedha nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na kusema kuwa waache mara moja kwakuwa ni mwizi.
Steve amekielezea kitendo hicho kama wizi usio na aibu kwa familia ya Sajuki iliyopo kwenye majonzi makubwa.
Ameongeza kuwa taratibu zote za kukusanya fedha zinaendelea msibani maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam huku yeye na Mike Sango wakihusika na ukusanyaji huo.
"SIJAGAWA PENZI KWA MUDA WAMIAKA KADHA..." MWASITI WA BONGO MOVIE
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHISHI 11:24 PMMWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Mwasiti Mohamed ‘Shishi’ amefunguka kuwa hajakutana na mwanaume kwa takribani miaka mingi iliyopita.
Shishi anadai kuwa tangu agombane na mpenzi wake ambaye hakumtaja miaka mingi iliyopita, hadi leo hamjui mwanaume.
“Haah! Aisee ni miaka mingi kwa kweli sijaduu, kila nikikumbuka yule mwanaume alivyonizingua, sikutamani tena tendo la ndoa,” alisema Shishi.
TUNDAMAN ALIZWA MILIONI 7 NA "JIMAMA" WAKIWA FARAGHA
Posted by Bigie habari za kitaifa, tundaman 10:55 PMMSANII Tundaman baada ya kumcheka mwenzake Matonya na kumuimba kwenye wimbo wake kuwa alifungiwa ndani na mwanamke na kulizwa shilingi milioni 6, hali kwake imekuwa mbaya zaidi ambapo inadaiwa kuwa hivi karibuni amekombwa milioni 7 na mwanamke mmoja aliyelala naye na kujikuta akiwa hana hata chenji mfukoni.
Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi kwa sharti la jina lake kutotajwa kilidai kuwa, msanii huyo alikuwa na sh milioni 7 ambazo alizipata kwenye moja ya show alizofanya hivi karibuni.
Mhabishaji huyo alisema kuwa baada ya kupata kiasi hicho cha pesa alisita kwenda kulala kwa rafiki yake Madee ndipo alipoamua kwenda kwa mwanamke huyo kwa lengo kutunza fedha hizo bila kuchukua tahadhari yoyote na fedha hizo, kitu ambacho kimempelekea kupoteza fedha zote huku mwenyewe akiwa kimya kwa hofu ya kuchekwa.
“Jamaa hadi leo kimya hafanyi tena mchezo wa kwenda kulala na demu na mshiko mrefu kwani kilichomkuta anajuta ni kwa nini alimuimba Matonya kwenye wimbo wake,” kilidai chanzo hicho.
Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi kwa sharti la jina lake kutotajwa kilidai kuwa, msanii huyo alikuwa na sh milioni 7 ambazo alizipata kwenye moja ya show alizofanya hivi karibuni.
Mhabishaji huyo alisema kuwa baada ya kupata kiasi hicho cha pesa alisita kwenda kulala kwa rafiki yake Madee ndipo alipoamua kwenda kwa mwanamke huyo kwa lengo kutunza fedha hizo bila kuchukua tahadhari yoyote na fedha hizo, kitu ambacho kimempelekea kupoteza fedha zote huku mwenyewe akiwa kimya kwa hofu ya kuchekwa.
“Jamaa hadi leo kimya hafanyi tena mchezo wa kwenda kulala na demu na mshiko mrefu kwani kilichomkuta anajuta ni kwa nini alimuimba Matonya kwenye wimbo wake,” kilidai chanzo hicho.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...













