NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
siasa 5:37 AM
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja na Mara.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisini kwake Dr. Sisti
Kariah amesema kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha
uandikishaji kwa BVR katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na
Mara zoezi ambalo lilitarajiwa kuanza leo na badala yake zoezi hilo
litafanyika kuanzia tarehe 16/06/2015.
Uamuzi wa kusogeza mbele unafuatia mabadiliko ambayo yanaendelea
kufanywa na Mipaka ya kiutawala ya kata, Vijiji, Vitongoji na Mitaa.
Uandikishaji kwa kutumia mfumo wa BVR unatoa fulsa kwa wananchi wote
wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za Mpiga watatakiwa
kujiandikisha upya.
Zoezi la Uboeshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga
hivisasa limefikia asilimia 50 kwa maana ya mikoa iliyofikiwa na zoezi
hilo nchini Tanzania.