MAC REAGAN AWALAANI WANAOZUSHA KIFO CHA VENGU.ADAI KUWA KWA SASA HALI YA VENGU INAENDELEA VIZURI


KUFUATIA kuzushiwa kwa kifo kwa msanii wa kundi la Orjino komedi Joseph Shamba ‘Vengu’, mmoja wao wa wasanii wa kundi hilo Alex Chamila amefunguka na kulaani uvumi huu.
Akiongea na Mpekuzi wetu,  Alex Chalamila ‘Mac Reagan’ anasema kuwa kila mara watu wanatumia muda mwingi kuwapigia wasanii wa kundi hilo kutaka kujua kifo cha Vengu.
“Si jambo ambalo linaweza kumfurahisha binadamu yoyote ambaye anauguza au akiwa na ndugu yake akiugua alafu anapigiwa simu na watu, eti kisa wanataka kujua kama kweli amefariki, kwanini basi mtu asiulizie  mgonjwa anaendeleaje zaidi ya kifo?,” anasema Mac Reagan.
Mac Reagan aliongeza kuwa , kwa sasa VENGU amepata ahueni na ameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi(ICU) na kuhamishiwa wodi ya Mwaisela ili kuendelea na matibabu katika Hospitali hiyo ya Taifa Muhimbili

Posted by Bigie on 9:04 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.