MALARIA KALI YAMTESA SHILOLE

AFYA ya staa wa filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ni ya kusikitisha  kwani kwa siku kadhaa amelala kitandani akisumbuliwa na ugonjwa usiokubalika wa malaria.

Akizungumza kwa tabu mbele ya Mpekuzi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Shilole alisema alizidiwa ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi Kinondoni, Dar es Salaam ambapo alilazwa siku nzima na kutundikiwa dripu za maji na dawa baada ya kugundulika kuwa ana malaria kali.

Alisema ugonjwa huo ulimpelekesha vibaya kutokana na kutougua kwa muda mrefu na kutokuwa na tabia ya kucheki afya mara kwa mara.

“Kwa sasa naendelea vizuri, lakini kiukweli hali yangu ilikuwa mbaya,” alisema Shilole na kuwashukuru wasanii wenzake wa Bongo Movie kwa upendo waliouonesha kwake.

Posted by Bigie on 10:34 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.