NDIKUMANA AMTAHADHARISHA MKEWE, UWOYA AJIANDAE KUPOKEA MAITI TATU...


SAKATA la  mume wa Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kutorokea kusikojulikana na mtoto wao kipenzi, Krish, linaendelea ambapo hivi sasa  mwanaume huyo amemtumia mkewe meseji ‘SMS’ ya kifo.

Habari ya kutoweka kwa Ndikumana na mtoto  ililipotiwa kuwa Alhamisi iliyopita Ndikumana aliondoka nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam na kwenda kwa mama wa Uwoya, Mbezi-Jogoo ambapo alimchukua mtoto huyo na mwingine ambaye ni wa kwake, aitwaye Baset kisha kutokomea.

Akizungumza na mpekuzi wetu, Uwoya alifunguka kuwa wakati akihaha kumpata mwanaye, aliishiwa nguvu alipopokea SMS kupitia simu ya  kiganjani iliyotumwa na Ndikumana ikimweleza kwamba ajiandae kuitiwa maiti tatu.

Aliposema maiti tatu alimaanisha moja ya kwake (Ndikumana), ya pili ya mtoto wao na ya tatu ni ya yule mtoto mwingine wa Ndikumana (Baset).

“Kiukweli simwelewi Ndikumana hata kidogo, kwa nini anitumie meseji ya aina hii ukizingatia yeye ndiye katoroka na mtoto?”

“Napata wakati mgumu sana katika maisha yangu, hapa nilipo presha tupu. Ndikumana ameninyima usingizi, silali namuwaza mtoto wangu, amenisikitisha sana, siwezi kuvumilia, lazima nimchukulie hatua za kisheria.”

Uwoya aliendelea kutambaa na mistari kuwa kitendo alichokifanya Ndikumana ni cha kinyama kwa sababu bado mtoto ni mdogo na anahitaji uangalizi wa karibu wa mama .

“Najua mwanangu anateseka sana bila hatia. Hata kama tuna ugomvi, haimhusu mtoto hata kidogo.”
 
Uwoya alipotakiwa kueleza wana ugomvi gani na mumewe, hakusema chochote kwa maelezo kwamba ni mambo ya kifamilia zaidi.

Uwoya ambaye ni moto wa kuotea mbali katika muvi za Kibongo, alikiri kuwa ujumbe wa mauaji aliotumiwa na Ndikumana umesababisha aongeze jitihada za kumsaka popote alipo kwa msaada wa jeshi la polisi na atakapompata atakuwa na kesi ya kujibu.

Habari za chini kwa chini zinadai kuwa tangu ndoa ya wawili hao ilipopigwa na kimbunga hivi karibuni, mambo hayajatulia, huku maneno yakienea kwamba bado Ndikumana ana kinyongo hivyo analipa kisasi.

Juzi, Jumatatu mishale ya saa 10:48 za jioni wakati gazeti hili likijiandaa kwenda mitamboni, zilitua habari kwamba, Ndikumana amemrudisha mtoto huyo.

Posted by Bigie on 1:39 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.