IZRAEL YADAI KUWA HAINA MPANGO WA KUISHAMBULIA IRAN KWA SASA
JAMII 8:35 PM
Waziri wa ulinzi wa Izrael ametamka ya kuwa mashambulizi zidi ya mitambo ya kinyuklia ya Iran hayapo kwenye meza yake na serikali haina mpango huo.
Waziri wa ulinza Ehud Barak alisema " uamuzi wa kuyashambulia maeneo yaliyo na mitambo ya kinyuklia nchini Iran ni kitu ambacho si cha ukaribu na cha kuzaniwa kwa sasa, hivyo na nisingependa kuwapa muda maalumu."
Hata hivyo Ehud Barak alishindwa kuelezea kama Iran inauwezo wa kutengeneza bomu la kinyuklia kwa kusema "sijui na siwezi kuthibitisha hilo."
Waziri wa ulinzi Ehud Baraka aliyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na radio ya kijeshi ya jeshi la Izrael.