NAJMA APATA NAFASI YA KUCHEZA FILAM MOJA NA MERCY JOHNSON

MWANADADA chipukizi katika tasnia ya filamu bongo, Najma Suleiman ‘Najma’, amesema amepata nafasi ya kipekee ya kucheza kazi moja na msanii kutoka Nollywood Nigeria anayekwenda kwa jina la Mercy Johnson, huku akiwa bado hajapewa jina kamili la kazi yenyewe.

Akizungumza na
mpekuzi wetu , juu ya harakati zake za mwaka 2012, msanii huyo alisema amekuwa katika maandalizi ya filamu lakini kubwa lililomfurahisha ni kupata bahati hiyo kama msanii kutoka Tanzania.

“Kuna kipindi nilikuwa nawasiliana na ‘Mercy’, kwa njia ya mtandao na nilikuwa nazungumza naye mambo mbalimbali kuhusu sanaa hivyo akanieleza kuwa akiwa anatatengeneza filamu yake ataweza kunitumia,”
alisema.

Najma alisema mbali na kwenda nchini Nigeria pia yupo katika maandalizi ya filamu yake ambayo itakuwa inaelezea mafuriko yalitokea mwishoni mwa mwaka jana ambayo yalisababisha watu wengi kukosa makazi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.

Posted by Bigie on 9:33 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.