WANAFUNZI WATATU UDSM WASHITAKIWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUPIGA KELELE NA KUFANYA FUJO CHUONI HAPO


WANAFUNZI watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na makosa ya kupiga kelele na kufanya fujo chuoni hapo.

Wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Christopher Mbusule (26), Wilson Bukosa (23) na Ben Stora (27).

Wakili Kaganda alidai kuwa Januari 11, mwaka huu, washtakiwa hao katika eneo la chuo hicho waliwafanyia fujo askari polisi na wanafunzi wenzao waliokuwa katika chumba cha mtihani kiitwacho Yombo.

Hata hivyo washtakiwa wote walikana mashtaka hayo na wakili Kaganda akasema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama iwapangie tarehe ya kuja kuwasomea maelezo ya awali.

Hakimu Lema akitoa masharti ya dhamana ambapo kila mshtakiwa alitakiwa awe na wadhamini wawili ambao mmoja wao angesaini bondi ya sh milioni moja.

Hata hivyo washtakiwa wote walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na akaamuru waende gerezani hadi kesi hiyo itakapokuja Januari 30, mwaka huu, kwa ajili ya washtakiwa kusomea maelezo ya awali.

Posted by Bigie on 2:32 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.