YVONE CHERRYL "MONALISA" ATOA SIRI YA KUSHIRIKI TUZO ZA KIMATAIFA
JAMII 6:34 PM
MSANII pekee anayeshiriki tuzo za kimataifa mara kwa mara Yvonne Cherryl ‘Monalisa‘, amewafumbua macho nyota wengine kwa kusema kuwa heshima anayoipata ya kushiriki tuzo hizo ni kutokana na ubora wa kazi zake pamoja na nidhamu aliyonayo ndani ya tasnia hiyo na nje ya filamu.
Msanii huyu ni moja kati ya nyota wenye nidhamu ndani ya bongo movie, na hata katika upande wa maisha yake ya kawaida, huku akiwa ni nyota pekee ambaye hana tabia zinazochangia kuvunjika kwa maadili.
Akizungumza na mpekuzi wetu kuhusu heshima anayoipata nje ya nchi, msanii huyo alisema kikubwa ni nidhamu aliyonayo kwani tangu aanze kucheza filamu hakuna mtu aliyewahi kuchukiana naye .Anaamini endapo tabia yake itakuwa kama ya nyota wengine basi heshima yake kama kioo cha jamii itashuka.
“Sidhani kama Watanzania watarufahi watakapo niona nimepiga picha za nusu uchi, au nafanya mambo ya ajabu kwa lengo la kutafuta umaarufu, najiheshimu sana na ndiyo maana kila wakati nakuwa mtu mzuri kwa mashabiki wangu wa ndani na nje ya nchi,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa wapo wasanii wa bongo movie ambao wanacheza filamu lakini hawatokuja kupata tuzo kwani tabia zao ndani ya filamu pamoja na maisha yao ni mabaya hivyo hawawezi kuitwa kwenye nafasi yoyote ya tuzo.
Mpekuzi wetu alitaka kujua ni nyota gani ambao katika maisha yao ya filamu hawawezi kupata tuzo hata wacheze filamu 1000 ambapo alijibu kuwa hawezi kuwataja majina kwani wanajijua na kitu kinacho wakwamisha ni tabia zao za kujiona wamefika.