ALICHOSEMA RAIS WA ZANZIBAR KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA.

.
Rais wa Zanzibar Dk. ALI MOHAMED SHEIN amelaani vikali vurugu zilizojitokeza Visiwani Zanzibar hivi karibuni na kusababisha uvunjifu wa amani, hivyo amewataka wananchi visiwani humo kuungana na kuacha kasoro zilizopo kati yao ili amani iendelee kuwepo.


Akizungumza na waandishi wa habari, wahariri na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. SHEIN amesema kuwepo kwa mikutano yenye sura ya dini lakini inahusu masuala ya siasa hasa Muungano ni uvunjifu wa amani na ndiyo sababu iliyosababisha vurugu visiwani humo na kutaka jambo hilo lisijirudie kwani limeonyesha ubaguzi na kujenga hofu kwa wananchi.


Amesema amekuwa na utaratibu wa kukutana na viongozi wa dini mbalimbali na kuzungumza kuhusu masuala ya ulinzi wa amani na kubainisha kuwa ataendelea na utaratibu huo ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa kisiwa cha amani.


“tumeshuhudia maandamano ya mikutano yenye sura ya dini lakini yenye ujumbe wa siasa, imefikia mpaka wameamua kuchoma moto majengo, wakachoma Makanisa ya ndugu zetu wakristo bila sababu yeyote ile, wamevunja maduka ya baadhi ya wenzetu raia wema, nimeshangazwa sana.. kuna uhusiano gani wa kuzungumzia muungano na kuchoma moto makanisa, kuiba vitu vya watu, kutukana na kutisha watu? haya ni kinyume na katiba yetu na sheria zetu” alisema Dr Chein.


kwenye sentensi nyingine Dk. SHEIN amewataka wananchi kutumia busara na kufuata taratibu zilizowekwa katika kutoa maoni ya katiba ili kuwezesha kupatikana kwa katiba bora kwa kurekebisha kasoro zilizopo.

Posted by Bigie on 8:41 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.