KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) YAWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WALIOHAMISHIWA MABWEPANDE

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo (kulia) akifafanua jambo wakati akitoa taarifa ya jinsi Serikali ilivyoshughulikia maafa ya mafuriko yaliyotokea kati ya tarehe 20-21 Desemba 2011 mkoani Dar es Salaam, katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, alipoiwasilisha kwa Kamati ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mh. Zainabu Vulu (hayupo pichani). Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Sylevester Rioba na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu wa Maafa (Operesheni na Uratibu), Nyanchaghe Nanai.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa (PAC), Bi Zainabu Vullu, wakati wakielekea kukagua makazi ya waathirika wa mafuriko ambapo maafa hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Mkoani Dar es Salaam kati ya tarehe 20-21Desemba 2011 yalisababisha vifo vya watu 41 na uharibifu wa makazi ya kaya 606.
Mmoja wa waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam kati ya tarehe 20-21 Desemba 2011 na kuhamishiwa Mabwepande, Nurdin Hamza akisisitiza juu ya mambo matatu ambayo serikali inatakiwa kuyaboresha katika makazi hayo, ambayo ni Maji, Afya na Umeme, ambapo serikali iliwahakikishia wananchi hao kuboresha na kukamilisha huduma hizo kwa muda muafaka.
Baadhi ya waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Mkoani Dar es Salaam kati ya tarehe 20-21 Desemba 2011 wakiwa katika mkutano wa (PAC).
Makamu Mwenyekiti wa (PAC) Zainabu Vullu akikagua moja ya hema la muathirika wa wa mafuriko, kushoto ni Mbunge wa jimbo la Msoma Mjini Mh. Vicent Nyerere ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Posted by Bigie on 9:22 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.