"BABA HATAKI NIVAE NUSU UCHI, NA MIMI SIWEZI KUVAA GAUNI UTADHANI NIKO KANISANI"....LINAH


Mwimbaji Linah ambae juzi alitangaza  kwamba ameamua kuwazawadia wazazi wake nyumba aliyoijenga Mpiji Mbezi Dar es salaam kwa thamani ya milioni 30 za kitanzania, amesema pamoja na wazazi wake kufahamu kwamba matunda hayo yametokana na muziki peke yake, amekubali kwamba baba yake mzazi mpaka sasa bado hakubaliani na mavazi anayoyavaa Linah.

Namkariri Linah akisema “nimejitahidi sana kuwaelezea wazazi wangu wanielewe litakapotokea tatizo lolote itakua ni bahati mbaya tu lakini sio kwa makusudi, baba anaona pia kwenye magazeti huwa navaa hivi najitahidi kumwambia hivyo ni vitu vya bahati mbaya huwa vinatokea na mimi kama msanii ndio maana tunakula tunaishi lakini ndio kazi

Mbali  na hayo Linah kasema “nyimbo zangu baba anazisikiliza na anazipenda na anakubali ninaimba kitu ambacho kipo, ila ubishi mkubwa kati yangu na yeye ni mavazi, kuna show na show.. siwezi kwenda kufanya show ufukweni alafu nimevaa magauni, show nyingine tunatakiwa kubang siwezi kuvaa migauni kama niko kanisani”
.

Posted by Bigie on 5:50 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.