PENZI LA NISHA NA NAY WA MITEGO LAZIDI KUOTA MIZIZI

SALMA Jabu ‘Nisha’ anayefurukuta kwenye tasnia ya filamu Bongo, ameibuka na kunadi uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwamba mambo yameiva na muda wowote atavutwa ndani.

Huyu hapa Nisha: “Mimi na Nay wangu sasa mambo safi. Muda wowote mnaweza kusikia mengine. Mama yangu amemkubali na amempokea kwa mikono miwili. Kikubwa  alikuwa hataki kusikia natoka na mume wa mtu.


“Ameridhia kwani hachagui kabila wala dini ilimradi awe siyo mume wa mtu. Kwa sasa Nay yupo kwenye shoo za Fiesta, akimaliza tutaanza taratibu za ndoa.”

Posted by Bigie on 1:59 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.