TAARIFA KWA UMMA JUU YA UHALALI WA MAUZO YA VOCHA YA TSH 450 TOKA VODACOM



 Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imekuwa na taarifa na malalamiko mbalimbali kuhusiana na mauzo ya vocha ya Tsh450 inayouzwa  kwa bei ya juu Tsh500 wakati vocha hizo kiuhalali zinauzwa kwa Tsh 450. 
 
Vocha hizi za Tsh450 zimetolewa katika soko ili kuwawezesha  wateja wetu kuwa na mawasiliano ya urahisi zaidi. Bei halali ya vocha hii ni Tsh450 kama ilivyo andikwa kwenye Vocha na tunawahimiza wateja wetu wanunue vocha hizo kwa bei halali  iliyotangazwa,siyo vinginevyo.
 
Tunashukuru kwa maoni yenu juu ya hili swala na tunafatilia kwa ukaribu zaidi kwa wauzaji wa vocha hizi kuhakikisha wanatoa huduma bora na ya uhakika kwa watejawetu na wananchi kwa ujumla.
 
Tafadhali shirikiana nasi kwa kutoa taarifmbalimbali hususani kuhusina na swala hili la vocha hizi za Tsh450 kupitia kurasa yetu ya facebook na Twitter.

Posted by Bigie on 12:58 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.