TAFF YAJIPANGA KUANZA KUTOA ADHABU KWA WAIGIZAJI WANAOVUNJA MAADILI YA KITANZANIA



SHIRIKISHO la filamu Tanzania TAFF, limetoa tamko kwa wasanii wake hasa wale wanaoendelea kufanya vitendo vya uvunjaji wa maandili kuwa wanasuburi sheria kutoka BASATA, ili waaze kuchukua hatua za kinidhamu.

Akizungumza na mtandao huu
,Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba, alidai kuwa wanasikitishwa na tabia ambazo zinanaendelea kufanywa na wasanii wake kwani vitendo hivyo vinawafanya hata wadau wa tasnia hiyo kuounguza kasi ya kununua kabisa filamu zao zinapotoka.

“Sisi kama TAFF tunasuburi sheria kutoka BASATA, acha waendelee kujiachia na tabia zao chafu, kwani baada ya sheria hii kutoka watakuwa matumbo joto na hatutafanya mchezo tutahukumu kila anayevunja sheria na kanuni,”
alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa sheria ambayo wanaisuburi kutoka BASATA ni ile ambayo itakuwa inatoa adhabu kwa wasanii ambao wanavunja maandili, kanuni zitakazojieleza ndani ya sheria hiyo na wengi wote ambao wataonekama kwenda kinyume.

Posted by Bigie on 1:52 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.