KESI YA LULU MICHAEL YAGONGA MWAMBA NA KUAMRIWA IANZE KUSIKILIZWA UPYA- KISUTU

KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayedaiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’ ambayo leo ilitakiwa kutolewa maamuzi ya umri na Mahakama ya Rufaa imerudishwa mahakama ya Kisutu kuanza upya.

Akitoa maamuzi hayo, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo yenye maamuzi ya mwisho hapa nchini, Zahra Marume amesema utaratibu uliotumika kuifikisha kesi hiyo mahakamani hapo ulikuwa na makosa hivyo kuamuru kesi hiyo kurudi mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam ili kuendelea na kesi ya msingi.

Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo jana Ijumaa Oktoba 5, 2012, jijini Dar es Salaam, Marume alisema, kwa mujibu wa sheria, jaji wa mahakama kuu, Dkt. Fauz Twaib alikosea kuamuru umri wa Lulu kuchunguzwa.

“Kama aliona kuna mapungufu, alipaswa kurejesha faili la kesi hiyo  Mahakama ya Kisutu kwa maelekezo na sio kutoa uamuzi kuwa umri wake uchunguzwe,” alisema.

Uamuzi huo umekuja mbele ya majaji watatu waliokuwa wakisikiliza pande mbili za mashitaka na utetezi kuhusu maombi ya upande wa mashitaka kutaka maombi ya Mahakama Kuu kutaka umri wa Lulu uchunguzwe yatupiliwe mbali.

Juni mwaka huu, mahakama kuu ya Tanzania iliamuru uchunguzi kuhusu umri halisi wa Lulu ufanyike kufuatia maombi ya upande wa utetezi.

Posted by Bigie on 7:10 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.