"SIWEZI KUTOA RUSHWA YA NGONO ILI NICHEZE FILAMU YA MTU"....MARTHA
BONGO MOVIE, habari za kitaifa, martha 7:09 AM

MSANII wa filamu Martha Nkunde ‘Martha’, ameuambia mtandao huu kuwa kamwe hawezi kushiriki kwenye filamu ya mtu kwa kutoa rushwa ya ngono, na kama hivyo ni bora akae nyumbani kuliko kujidhalilisha na mwisho wa siku azungumziwe kuwa ni muhuni.
Martha alifunguka na kudai kuwa kwa upande wake ni heri asifanye filamu kwani kitu kibaya ni kujirahisisha na kama una kipaji huna sababu ya kuruhusu kuchezewa ovyo.
Martha alifunguka na kudai kuwa kwa upande wake ni heri asifanye filamu kwani kitu kibaya ni kujirahisisha na kama una kipaji huna sababu ya kuruhusu kuchezewa ovyo.
Hata hivyo aliongeza kwa tangu alipoingia kwenye tasnia hiyo hakuna mdau wa filamu aliyewahi kumuomba rushwa ya ngono kwa lengo la kupata nafasi ya kushiriki kwenye filamu.