PENZI LA NEY WA MITEGO LAMCHANGANYA BINTI WA 20 PERCENT


Asfa Omary Neema
 MWIGIZAJI wa kike katika ya tasnia Bongo Movies Asfa Omary Neema 20% ameshindwa kuficha hisia zake pale alipodai kuwa pamoja na umri wake mdogo anamzimia sana msanii wa Bongo fleva, Ney wa Mitego.

 "Siyo siri ,nampenda sana Ney wa Mitego na natamani awe mume wangu wa ndoa hata kesho kama akikubali, kama ingekuwa wasichana tunaruhusiwa kuwatongoza wanaume na kuolewa nao basi mimi ningekuwa wa kwanza kwa Ney, ana mvuto na shababi"  Neema 20%.

Neema ni msanii aliyevuma na kuibuka kupitia filamu ya 'Furaha Iko Wapi' iliyotungwa na msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamis Kinzasa "20 Percent" amedai kuwa anampenda mwanamume anayejiamini na kuwa mtanashati...


Anadai kuwa hizo sifa anaziona kwa  msanii Ney  pekee na si mtu mwingine, na atafanya kila juhudi ili aweze kuishi na msanii huyo

Posted by Bigie on 6:20 PM. Filed under , , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.