REDSON ALIKATAA DILI LA KUPIGA PICHA CHAFU.....


Redsan

Msanii wa nchini Kenya Swabri Mohammed maarufu kama Redsan amesema alikataa deal la kupiga picha za utupu kwa sababu hiyo sio tabia yake.

Katika interview aliyofanya na mtangazaji wa radio moja nchini Kenya aitwae Adelle ambae alikuwa anamuuliza kuhusu maisha yake, mtangazaji huyo alimuuliza Redsan kama alishawahi kupiga picha akiwa mtupu, na jibu la Redsan liliambatana na taarifa ambayo iliwashtua mashabiki wengi.

“Nakutaka” hit maker alisema hajawahi kupiga picha akiwa mtupu na hatafanya hivyo, kaisha akaongeza kuwa actually hivi karibuni jarida la Fitness walipropose nipige picha nikiwa bila nguo, lakini nikawaambia hiyo sio style yangu.”

Watu maarufu wengi hasa waimbaji na wasanii wa kuigiza wamekuwa wakipiga picha zinazoonesha wakiwa nusu uchi ama hata wako watupu, kutokana na kuwa siku za karibuni Kenya kumekuwepo na baadhi ya majarida yanayotoa mpunga mrefu kwa ajili ya matangazo ya picha za aina hiyo. 
 
Tunaweza kusema kwa kulingana na maadili ya kiafrika basi Redsan ni mfano wa kuigwa.

Posted by Bigie on 2:38 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.