MUME AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MKEWE


KIZITO Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa Msili B jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi namba 5A baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji ya moto mwilini.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii huku akiwa katika hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38) kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila alipojerea nyumbani.


“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke wangu hakuwa katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa, nikajiuliza kulikuwa na nini?

“Hayo yote yalipokuwa yakiendelea,  jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa nimelala nilishitukia  mke wangu akiingia chumbani na chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni. 


Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .

“Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye anayenisaidia,”  alisema Mahamba.

Posted by Bigie on 10:48 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.