NDOA YA AUNT EZEKIEL YAINGIA DOSARI BAADA YA TETESI KUSAMBAA KUWA MUME WAKE ANASAKWA NA POLISI


BAADA ya ile harusi ya msanii maarufu wa filamu bongo Aunty Ezekiel kufungwa huku mastaa wakimsapoti shangwe, ishu nzito imeanza kujitokeza kuwa mume wa msanii huyo hawezi kuonekana kwenye ardhi ya bongo siku za usoni, kwa madai kuwa anatafutwa na jeshi la Polisi.

Upekuzi uliofanywa na mwandishi wetu
wa kutaka kubaini kwa nini bwana harusi hakutaka kumaliza ishu hiyo mwenywe, ndipo taarifa hizo zilipobainika kuwa jamaa huyo kuna ishu nzito aliyoifanya bongo na ndiyo sababu kubwa ilimfanya asije hata kuonekana kwa wakwe zake.

Chanzo cha habari kilichozungumza namtandao huu 
   kimedai kuwa awali kabisa kabla ndoa haijafungwa jamaa alitakiwa kuja nnchini lakini hakuweza kukubali kwa kujua kuwa anatafutwa na polisi na endapo akionekana atakuwa kwenye matatizo.

Mtu huyo aliongeza kuwa kuna uwezekana hata wanafamilia wa msanii huyo wakashindwa kumuona kabisa mwanaume huyo kwani ishu inayoendelea ni kwamba jamaa ameshatoa taarifa kuwa hawezi kuja nchini na mtu anayemtaka basi ni lazima apange safari amfuate.

Posted by Bigie on 9:47 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.