"MAMA USIJE KWANGU BILA TAARIFA.....VINGINEVYO WALINZI WATAKUTIMUA".......WEMA SEPETU


KITENDO cha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuwaambia walinzi wake kuwa kama hajatoa maagizo yoyote kwamba mama yake, Mariam Sepetu anakuja, akifika mlangoni asifunguliwe kimewashangaza wengi.


Awali, Wema alieleza kuwa, ameweka utaratibu wa watu kuonana naye na kwamba wale watakaokwenda kwake bila taarifa watakuwa wanaishia getini.

Maelezo hayo yalimfanya mwandishi wetu amuulize kama hata mama yake akienda kwake bila ‘apointimenti’ hawezi kuingia ndani ambapo alisisitiza kwa kusema kuwa, utaratibu huo ni kwa watu wote akiwemo mzazi wake huyo.


“Akija bila taarifa hawezi kuingia ndani. Si yeye tu, hata dada yangu, rafiki yangu yoyote yule, meneja wangu hata wewe kama sijatoa maagizo kwa walinzi basi ujue utaishia nje na ukinipigia simu huwa sipokei,” alisema Wema.


Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya watu kumshangaa kwa kusema kuwa, utaratibu huo si mzuri kwani kufikia hatua ya kumtaka hadi mama yake aweke apointimenti ndipo amtembelee ni kutafuta laana.

Posted by Bigie on 2:18 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.