BABY CANDY, SKAINA NA JACK CHUZ WAGOMBEA PENZI LA TIMBULO....
habari za kitaifa, picha za utupu 4:40 AM
MASTAA wasichana wa mjini, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz, Skyner Ally ‘Skaina’ na Baby Candy wamejikuta wakirushiana matusi kupitia mtandao wa kijamii wa BBM kisa kikiwa ni msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo.
Aliyelianzisha bifu hilo ni msanii mmoja rafiki yao na akina Baby Candy ambaye alianza kwa kumtumia ujumbe wa matusi Skaina na kumwambia anaiba mabwana wa wenzake akimaanisha anataka kumuiba Timbulo.
Baada ya matusi kutua kwa Skaina aliyetuma ‘pini’ ya Timbulo mtandaoni akimuombea marafiki, Baby Candy naye aliamua kumtupia Skaina maneno makali akimalizia kwa kumwambia kuwa anaingilia vitu asivyovijua.
Ilifahamika kuwa baada ya kusoma ujumbe wa Baby Candy, Skaina alimporomoshea matusi mazito ambayo hayaandikiki akimalizia kwa kumwambia kuwa hana lolote bali anatafuta tu ustaa mtandaoni.
![](http://1.bp.blogspot.com/_MsaNQZtvB5E/StANlDhWFgI/AAAAAAAAAKA/8p5PORokslI/S220/normal_HNH_9244-sapa0207.jpg)