KESI YA LULU MICHAEL YASAJILIWA RASMI MAHAKAMA KUU
habari za kitaifa, LULU MICHAEL 11:32 PM
Kesi ya mauaji ya kutokukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael `Lulu’, imepokelewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa namba 125 ya mwaka 2012.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mahakamani hapo, kesi hiyo imepokelewa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na inasubiri kupangiwa Jaji na tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, kwa kukusudia lakini baada ya upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi alibadilishiwa mashitaka na kuwa kuua bila kukusudia.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Augustina Mmbando, katika hatua za awali na Lulu hakuruhusiwa kujibu mashitaka yanayomkabili kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kwa mujibu wa sheria, kutokana na Lulu kushitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, anaweza kupata dhamana.
Posted by Bigie
on 11:32 PM.
Filed under
habari za kitaifa,
LULU MICHAEL
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0