MZEE MAJUTO AJIPANGA KUTOKA NA "PATASHIKA" AMBAYO NI ZAIDI YA KOMEDI
BONGO MOVIE, habari za kitaifa, MAJUTO 2:21 AM
MCHEKESHAJI mkongwe, Amri Athuman ‘King Majuto’ hivi karibuni ataanza kuonekana kwenye kazi mpya iitwayo “Patashika”
Katika kazi hiyo iliyojaa vichekesho vya kuvunja mbavu, Majuto atacheza kama baba wa familia mwenye vibweka vingi vya kustaajabisha, vinavyowaacha watu hoi kila siku mtaani kwao.
“Nategemea kufanya kitu cha tofauti ili mashabiki waweze kujua mimi ninaweza kuigiza ndiyo maana ninaigiza kama baba wa vibweka kwahiyo wadau wangu wategemee vimbwenga vya kustajabisha” alisema gwiji huyo wakuchekesha.
Mbali ya Majuto katika picha hiyo pia inawashirikisha nyota wengine ambao ni wakonnge kwenye Nyanja za uchekeshaji wakiwemo Pembe, Senga, Kingwendu, Full Tank na Difenda.
Kazi hiyo imepangwa kuingia sokoni hivi karibuni, ambako itapatikana mikoa yote hapa nchini, kwenye VCD pamoja na DVD
Posted by Bigie
on 2:21 AM.
Filed under
BONGO MOVIE,
habari za kitaifa,
MAJUTO
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0