Bunge la Ufaransa laidhinisha ndoa za jinsia moja na kuasili watoto

Bunge la Ufaransa limeupitisha mswada unaoruhusu watu wa jinsia moja kuoana na pia kuwa na haki ya kuasili watoto.
Wabunge wa chama cha Kisoshalisti cha rais Francois Hollande, wameupitisha mswada huo kupitia kikao cha bunge.

Hatua hii inaifanya Ufaransa kujiunga na orodha ya nchi nyingine duaniani, nyingi zikiwa za Ulaya ambazo zinaruhusu ndoa za jinsia moja na kuasili watoto kwa wanandoa hao.

 Hatua hiyo, imekuja baada ya maandamano makubwa katika wiki za hivi karibuni yaliyokuwa yakipinga mswada huo uliopewa jina la “ndoa kwa wote”. 

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa Wafaransa wengi wanaunga mkono ndoa za jinsia moja.

Posted by Bigie on 4:23 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.