"WALIONICHEZEA INATOSHA....NAJUTA KUZOAZOA WANAUME OVYO"..NISHA WA BONGO MOVIE



MWANADADA anayeuza nyago kwenye soko la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’  amedai kuwa amekoma kuzoazoa wanaume bila kufanya uchunguzi. 

Nisha alimwambia mwandishi wetu kuwa, amekuwa akiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume mbalimbali bila kuwachunguza na matokeo yake imekuwa ni kuchezewa kisha kutoswa.

“Hii tabia ya kuzoazoa wanaume bila kuwachunguza inabidi niiache, mwanaume ambaye nitakuwa naye kuanzia sasa ni yule ambaye nitakuwa nimejiridhisha kuwa ananipenda kwa dhati. Kinyume chake bora niwe singo...” alisema Nisha.


Msanii huyo aliongeza kuwa kuna wanaume wanampotaka msichana hasa staa, hutumia gia ya kuoa lakini wakikubaliwa kisha kutoa penzi huingia mitini ndiyo maana ameamua kuwa makini na suala hilo.

Posted by Bigie on 2:14 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.