KOCHA WA AZAM FC APEWA ADHABU KALI BAADA YA KUVUA BUKTA UWANJANI


.
Kocha wa club ya soka ya Azam FC Stewart Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh 500,000 kwa kushusha bukta aliyokua ameivaa wakati akimlalamikia mwamuzi msaidizi kwenye mechi ya Azam na Kagera Sugar kwenye ligi kuu ya Tanzania bara January 26 2013 Chamazi, Mbagala Dar es Salaam.

Adhabu imetolewa na TFF baada ya kukutana  na kupitia ripoti za michuano ya Ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza.

Kocha Msaidizi wa Mgambo Shooting Denis Mwingira ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi wa mechi na Mtibwa Sugar october 2012.
 
Ally Jangalu akiwa ni kocha msaidizi wa Polisi ya Moro nae amepigwa faini ya laki tano baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga kwa sauti kubwa maamuzi ya refa November 2012.

Posted by Bigie on 7:35 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.