NOKIA YAZINDUA SIMU INAYOTUNZA CHAJI KWA MWEZI MZIMA NA GHARAMA YAKE NI SH. 30,000



Baada ya Nokia 1100 huenda Nokia 105 ikaja kuwa simu maarufu zaidi hasa kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Hii ni baada ya kampuni hiyo ya simu kuzindua simu hiyo yenye uwezo wa kutunza chaji kwa siku 35 kila unapochaji.


Simu hiyo imetengenezwa maalum katika maeneo ambayo umeme hakuna ama unasumbua lakini pia kama ‘backup phone’ pale zingine zinapozima.
nokia
Ikiwa inatarajia kuingia sokoni wiki kadhaa zijazo, Nokia 105 ambayo bei yake ni paundi 13, sawa na shilingi 30,000 za Tanzania pia ina tochi na FM radio.

Posted by Bigie on 3:20 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.