"SINA UHUSIANO WOWOTE NA MASTER J...MPENZI WANGU ATATAMBULIKA BAADA YA KUFAHAMIKA KWA WAZAZI"...SHAA

Shaa na Master J.Hii interview ya Shaa kwenye Leo Tena ya Super Brand Clouds FM......

Ni kuhusu alichosema kuhusu taarifa za uhusiano wake na Producer Legend Tanzania Master J, ilikua ni interview ambayo hata mimi nilienjoy kuisikiliza manake Dina Marios na Shaa na wengine waliokuwepo studio walikua wamechangamka sana alafu Shaa alijiachia vizuri pia.
 
Alichojibu Shaa kwenye maswali ya ndio au hapana ni hapana, akisema “Ndugu mtangazaji hapana, hatuna uhusiano wowote”

Kwenye mstari mwingine Shaa alisema mpenzi wake atatambulika baada ya wazazi wake kumfahamu na kupokea mahari, baada ya hapo sasa kadi za mwaliko ndio zitaweka ukweli ambao wengi wanataka kuujua.

Basi baada ya kusoma hii stori ya Shaa natumia nafasi hii kukualika kuisikiliza hii hit song ya Promice ambayo iliandikwa na Barnaba Boy, support cha home.



CREDIT: MILLARDAYO

Posted by Bigie on 1:16 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.