"WASANII WADOGO NI WADAU WA BIASHARA CHAFU YA NGONOI KWA VIGOGO NA MAANA WANAJIFANYA WANAPESA CHAFU"...CATHY ATOBOA JIPU


MWIGIZAJI zao la Kundi la Mambo Hayo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa swali alilokuwa akijiuliza juu  ya wasanii wadogo kuwa na fedha nyingi za ghafla limepata jibu, kumbe zinatokana na wasanii hao kujiuza kwa vigogo. 

Akiongea na  mwandishi wetu, Cathy alisema tukio la Jack wa Chuz kunaswa hivi karibuni akienda kuuzwa, linatoa picha mbaya kwa wasanii wa kike hivyo anawasihi wote wenye tabia hiyo waache mara moja.

“Pato la kazi yetu ya filamu tunalijua, wengi tulikuwa tunawaona wakimwaga fedha nyingi kwenye sherehe mbalimbali pasipo kujua wapi wanazipata fedha hizo. Wasanii wanatakiwa kubadilika ili tuheshimike,” alisema Cathy.


Jumatano ya Februari 20, mwaka huu, Jack wa Chuz aliripotiwa na Gazeti la Risasi Mchanganyiko kuwa alinaswa akijiuza kwenye hoteli moja iliyopo Ubungo, Dar.

Posted by Bigie on 5:45 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.