AJALI YA BASI YAMUUA MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM )


Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Mohamed Trans likitokea Dar es salaam kwenda Dodoma baada ya kupata ajali katika eneo la Kiegea, Gairo barabara ya Morogoro-Dodoma.

Aliyefariki ametambulika kuwa ni Bernadeta Minja aliyekuwa Mhadhiri katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Idara ya Uchumi na Biashara ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) aliyekuwa safarini na mfanyakazi wake wa ndani.

Kwa mujibu wa Josephat Lukaza  shughuli za msiba zinaendelea huko Kisasa, Dodoma alipokuwa akiishi marehemu.

Posted by Bigie on 10:21 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.