J MARTINS AFANYA COLLABO NA OMMY DIMPOZ, MWANA FA NA AY
habari za kitaifa 1:07 AM
Kuanzia kushoto ni Mwana FA, AY (katikati), Ommy Dimpoz, J Martins na Marco Chali wakiwa kwenye studio za MJ Records
Mwanamuziki na producer mahiri wa nchini Nigeria, Martins Okey Justice aka J Martins yupo nchini na amefanya collabo na Mwana FA, AY na Ommy Dimpoz.
Inavyoonekana staa huyo amewashirikisha AY na Mwana FA kwenye wimbo mmoja uliotayarishwa na Marco Chali kwenye studio za MJ Records.
“Confirmed now @Realjmartins ft on @AyTanzania and @MwanaFA New Single coming out soon,” imesomeka tweet moja.
Pia Ommy Dimpoz amemshirikisha staa huyo kwenye wimbo wake. “Finally @ommydimpoz did the Song with @Realjmartins (J.Martins) pic after the session,” imesomeka tweet nyingine ikiwa pamoja na picha.
