UCHAMBUZI WA VIDEO YA UTEKAJI WA LWAKATARE
Posted by Bigie
habari za kitaifa
11:33 PM
Mambo kadhaa ya kutafakari katika 'VIDEO ya Lwakatare':
- Video imechukuliwa tarehe 28-12-2012 baada ya sikukuu ya Krismasi; kwanini ije kutolewa miezi 3 baadae baada ya tukio la kuteswa Kibabanda?
- Mhusika kuweka hiyo video (BUKOBA BOY) amejiunga na YouTube tarehe 11-03-2013, na tarehe hiyohiyo akaweka hiyo video ambayo aliichukua tarehe 28-12-2012... Kama analipenda taifa hili, kwanini asingeweka mapema kabla na pengine Kibanda angeepukana na madhira yaliyomkuta?
- Katika dakika ya 16 na sekunde ya 55 ya video hii, Lwakatare anasema "either, nilivyopewa na kuistudy hii homework"; ina maana kuna mtu kamtuma? Ni nani?
- katika dakika ya 17 sekunde ya 32 lwakatare anasema" kama huyu mtu anakua na sehemu nyingi sasa tutatrace ngapi, lazima hawe na sehemu moja specific kuwa hakosi" jamani tujuzane hivi mtu anaepanga mauaji anachagua sehemu kweli ? mbona mwangosi aliuliwa kwenye mikono ya polisi inamaana huwa ndio ilikua sehemu yake ? mbona kijana kwenye maandamano alikufa kwenye mkutano inamaana morogoro kila siku palikua na mikutano na marehemu alikua ndio sehemu yake ?
- na mwisho kwanini video imekatiswa katikati ? je kuna matukio mengine yatafanyika alaf ndio waje na video ya 6 maana hiyo ni video ya 5 ?
- mwanzo kabisa ya video wanarekebisha mic, na mchukua video anasema "tuta-note upya hapo" inamaana kuna marekebisho ya kubadiri camera yalifanyika hata video inavyoanza tunaona kabisa walikua kimya.
TUSUBIRI MAJIBU YA POLISI

Posted by Bigie
on 11:33 PM.
Filed under
habari za kitaifa
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0