ZAIDI YA WANAFUNZI 387 WA REGINAL MENGI WAMESHINDWA KUENDELEA NA MASOMO



Zaidi ya Wanafunzi 387 wa Shule ya Msingi REGINALD MENGI iliyopo Sinza Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wameshindwa kuendelea na masomo baada ya uongozi wake kuifunga shule hiyo kufuatia choo chake kuvunjika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo.

Akizungumza na CLOUDS FM Mwalimu Mkuu wa shule hiyo JUVENALI MUTTA amesema, wamelazimika kuifunga shule hiyo kwa kuhofia wanafunzi kutumbukia kwenye choo hicho huku wakiepusha kutokea kwa magonjwa kama kipindupindu ikiwa watoto wataanza kujisaidia ovyo.


Mbali na hatua hiyo Mwalimu MUTTA, amesema tayari wameshatoa taarifa kwa uongozi wa Manispaa ya Kinondoni ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.


Ili kupata ufafanuzi juu ya hatua ambazo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhusiana na shule hiyo kufungwa kwa ukosefu wa vyoo tumezungumza kwa njia ya simu na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni YUSUF MWENDA…


Uchunguzi uliofanywa  umebaini kuwa licha ya choo hicho kuvunjika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, pia suala la ujenzi usiozingatia viwango limechangia kutokea kwa uharibifu huo.


CLOUDS FM imeshuhudia choo hicho kujengwa kwa matofali ya nchi tano badala ya sita kama inavyopendekezwa na Bodi ya Usajili Makandarasi nchini CRB ambayo yamesimamishwa badala ya kulazwa.

Posted by Bigie on 4:19 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.