KIJANA WA JORDAN AJILIPUA MOTO BAADA YA KUKATALIWA KUONANA NA WAZIRI


Kijana mmoja nchini Jordan ambaye siku chache zilizopita alikataliwa kuonana na Waziri wa Ustawi wa Jamii wa Jordan na kuamua kujiteketeza, amefariki dunia hii leo kwenye hospitali ya serikali  mjini Amman.

Kijana huyo yatima aitwaye Ahmad Rubain  mwenye umri wa miaka 23 ambaye siku ya Alhamisi iliyopita alitaka kuonana na Waziri wa Ustawi wa Jamii na kumuelezea matatizo na hali ngumu ya maisha inayomkabili, aliamua kujiteketeza moto mbele ya jengo la wizara hiyo baada ya juhudi zake za kutaka kuonana na waziri kugonga ukuta.
 

Msemaji wwa Hospitali ya serikali ya al Bashir mjini Amman amesema kuwa, asilimia 90 ya mwili wa kijana huyo ilikuwa imeteketea. Hili ni tukio la tano la kujichoma moto  katika kipindi cha miaka miwili nchini humo. 
 

Ni miaka miwili na nusu sasa Jordan inakabiliwa na wimbi kubwa la maandamano ya wananchi wanaotaka yafanyike marekebisho ya kisiasa, kiuchumi na mapambano dhidi ya ufisadi nchini humo.

---
Waviti via Radio Tehran

Posted by Bigie on 2:52 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.