CLINTON AMPONGEZA RAIS KAGAME.....ANADAI KUWA TUHUMA DHIDI YAKE HAZIJATHIBITISHWA MAHAKAMANI


Aliyekuwa rais wa marekani Bill Clinton amempongeza rais wa Rwanda Paul Kagame kwa  mafanikio ya  nchi yake  licha ya madai kwamba amekuwa akiunga mkono makundi ya waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo yanakiuka haki za kibinadamu.

Bwana Clinton amesema katika mahojiano na BBC kwamba madai hayo ambayo Rwanda inayakataa hayajathibitishwa mahakamani.
 
Pia alisema kuwa kuna changamoto kubwa katika mpaka wa Rwanda na Congo, kwani una watu chungu nzima ambao walihusika na mauaji ya halaiki miaka ya tisini.
 
Lakini bwana Clinton amesema kuwa anathamini serikali ya Rwanda kutokana na mafanikio ya kiuchumi yalioafikiwa chini ya rais Kagame.
 
Kiongozi huyo amekuwa akizuru mataifa ya Afrika pamoja na mwanawe Chelsea ili kujionea miradi ya wakfu wake.

Posted by Bigie on 4:34 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.