Mayasa awashangaa wanaodai kuwa ameolewa.....Asema yeye yupo Single na hahitaji ndoa kwa sasa maana bado ni mdogo sana
habari za kitaifa 3:26 AM
Msanii wa kike wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ( Maya ) amefunguka kuwa wale waliozusha kuwa amechumbiwa ni wanafiki na watasubiri sana mpaka wazeeke kwani suala la ndoa kwake bado halipo leo wala kesho.
Akiongea na mpekuzi wetu, mrembo huyo amedai kwamba uvumi ulionenezwa kuwa amechumbiwa ulikuwa una lengo la kumchafua na kumjaza mikosi ya kupendwa na wanaume.
"Nawashangaa wanaohangaika kuumiza midomo yao wakiwatangazia watu eti nimechumbiwa. Mimi nipo single na sihitaji kuolewa kwa sasa.
"Nahitaji mpenzi wa kufarijiana tu maana ndoa ni kifungo ambacho nadhani sipo tayari kukitumikia katika umri mdogo kama huu"
Posted by Bigie
on 3:26 AM.
Filed under
habari za kitaifa
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0