Wanawake Acheni Vigenge Vya Umbeya Na Kuwa Magolikipa Kwa Wanaume: Happy Nyatawe
Happy Nyatawe, udaku 5:38 AM
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Happy Nyatawe ambaye pia ni mfanyabiashara amewaasa wanawake wenzake kuacha kuwa magolikipa kwa wanaume na pia kuacha umbeya na badala yake wajikite katika kazi ili kujiletea maendeleo.
Akizungumza na Mpekuaji, Happy amesema:
"Nashangaa wanawake ambao mpaka karne hii wanategemea wanaume Kwanini siku moja na wewe mpenzi wako au mumeo asifurahie msaada toka kwako ?
"Wanawake tunaweza kataa u-golikipa na vikao vya umbeya mitaani, u-busy unaepusha mambo mengi sana .Tuwe bize kusaka pesa na si kusuta watu.
"Mimi mbali na biashara yangu muda mwingi napenda kupumzika nyumbani na kuangalia movie, yaani kazi za wenzangu na endapo itatokea msiba au sherehe hujumuika na wenzangu lakini naogopa sana kusutwa ndo maana sipend vigenge"
Posted by Bigie
on 5:38 AM.
Filed under
Happy Nyatawe,
udaku
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0