LINEX AMVISHA PETE MCHUMBA WAKE AMBAYE NI MZUNGU
Posted by Bigie habari za kitaifa, LINEX 5:11 PM| Mambo ya madini |
![]() |
| Wifi yetu katika pose |
![]() |
| Wapendanoooooooo safi sana |
![]() |
| Full kuringishia madini!! |
Weekend hii, mtu mzima Sunday Mjeda aka Linex aka Mr VOA (Voice Of Africa),alifanya yake kwa kumvisha pete mpenzi wake, ambae ni ambae ni mwenyeji wa Finland anaeitwa Suvi.
According to sources Linex aliamua kufanya kimya kimya tena wakiwa wawili tu, kwasababu hakutaka kujionyesha, na anaamini ile ni kitu very personal haikuhitaji manjonjo mengi.
Well hongera zao na tunawatakia kila la kheri.
"MABINTI WA KIBONGO WALIKUWA WAKINITESA NA KUNIKIMBIA...SASA NINA TOTO LA KIZUNGU. MWENYE UBAVU WA KUNINYANG'ANYA AJITOKEZE"...LINEX
Posted by Bigie habari za kitaifa, LINEX 7:58 PM-----
Kama unakumbuka vizuri, miezi kadhaa iliyopita, baada ya kuandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa anamsichana mwingine, na yeye kuruka futi mia na kusema bado yupo na mpenzi wake wa kizungu "Suvi" ambae ndio kila kitu kwake....
Leo hii Linex amethibitisha kuwa mambo yao hakuna anaeweza kuyaingilia..ukimsikiliza kwa makini utagundua kuwa anajiami sana kwa mpenzi wake huyo na ndo maana anajaribu kukuambia kuwa atakua ana matatizo kama kuna kvuvi atakae weza kutupa nyavu baharini na kumvua mpenzi wake wa sasa.
"kama kuna mvuvi atatupa nyavu kumvua huyu shemeji yenu wa sasa hivi basi ntakua nina tatizo, kwasababu maisha yangu mengi, nafkiri labda kwa sababu ya the way i was living, sababu unajua mi nataokea mtaani sasa labda the way nilivyokuwa naishi ilikua inafikia point watoto wa kike wanachoka maisha yangu ya mtaani na nini, so wanaamua kunichoka na wanaamua kuniacha na kuanza na maisha mengine,...
So hakuna jambo jipya kwenye swala la kupenda kwangu mimi yaani ...mi sina kinyongo na mvuvi ambae atatupa nyavu baharini na akafanikisha kumvua samaki ambae mi nilikua napenda kumuona aendelee kuwa baharini akifanya maswala yake".
WOKOVU WAMSHINDA STARA THOMAS NA SASA AMEAMUA KUIRUDIA BONGO FLEVA JAPO ALIIKIMBIA
Posted by Bigie habari za kitaifa, LINEX, stara thomas 5:33 PMNinauhakika utakua unaikumbuka ile stori ya mwimbaji wa bongofleva Stara Thomas kutangaza kuokoka na kuachana kabisa na muziki wa bongofleva, badala yake atakua anafanya gospel.
Japokua alitangaza kuwepo kwenye gospel rasmi baada ya kuokoka, Stara aliwahi kuweka wazi kwamba wasanii wa gospel hawana upendo na umoja, yani ni afadhali wasanii wa bongofleva mara mia manake amelishuhudia hilo kwa macho yake na wala sio kuhadithiwa.
Alichosema Linex ni kwamba wimbo huo wa bongo fleva umeshakamilika na kinachosubiriwa ni taratibu zilizopangwa za kuuachia, na kwa mujibu wa Linex ni kwamba Stara Thomas mwenyewe ndio alimpigia ili wairekodi hiyo kolabo ya bongofleva.
AMINI NA LINEX WAUNGANA TENA NDANI YA "USIKU WA MTIMA WANGU"
Posted by Bigie amini, habari za kitaifa, LINEX 12:59 AMBaada ya kufanya show kali katika fainali za BSS mwishoni mwa mwaka jana na kuzua mjadala kama wapenzi hawa wa zamani wamerudiana, wasanii wa THT Amini na Linah wanatarajia kufanya show nyingine pamoja huko Kigamboni, Dar es Salaam waliyoipa jina la ‘Usiku wa Mtima Wangu’.
Show hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Club Kakala siku ya Jumamosi ya January 5 ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 6,000 tu.
Wasanii hao kwa sasa wana wimbo mpya uitwao Mtima Wangu unaofanya vizuri kwenye vituo vya radio.
LINEX ASHITAKIWA KWA KUMPIGA KOFI LA KWELI MREMBO ALIYECHEZA NAYE VIDEO YA AIFOLA
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, LINEX 1:03 AMHiki kinaweza kuwa kituko cha mwaka kwenye muziki wa Bongo Flava. Mrembo aliyeigiza kwenye video ya Linex Aifola, ameamua kumfungulia RB msanii huyo baada ya kumpiga kibao cha kweli kwenye video hiyo.
Katika video hiyo Linex anaonekana akiwa amekaa kwenye kochi na kuanza kukagua simu ya mchumba wake Aifola ambaye humo ameigiza Janeth Bundala na ndipo alipogundua kuna meseji za kimapenzi anazotumiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kuchukia na kumpiga kofi kali la shavuni.
“hahhahahahhahaha frm no where eti janeti aka aifola kanipigia leo kaniambia kanichukulia R B kwa kofi nililompiga wakati tunaigiza hahah kama kachelewa hv,” aliandika Linex jana kupitia Facebook.
“Sijajua alikua anatania but ndo kitu alichoniambia muda si mrefu nimekia nacheka tu. Nimemsikia live radion anataka kulipwa aseeee kumbe anamaanisha. Nimeshaongea nae na kesho ndo nakutana nae rasmi ntajua anatakaje na ntamalizana nae.”
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...






