:TATOO ZA JINA LANGU ALIZOJICHORA MCHUMBA WANGU ZINADHIHIRISHA JINSI ANAVYONIPENDA"...ROSE NDAUKA
Posted by Bigie habari za kitaifa, rose ndauka 3:39 AM
MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka afunguka juu ya tatoo alizochora mchumba wake Mariki Bandawe, zinazoonyesha mchoro wa kopa . Alisema kupitia mchoro huo ni dhahiri kuwa mchumba wake amedhihirisha kuwa na mapenzi ya dhati
Rose alilazimika kufunguka juu ya hilo baada ya kupokea maswali mengi kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii 'Facebook' baada ya kuituma picha hiyo inayomuonyesha mchumba wake akiwa na mchoro kwenye bega lake la kushoto
Akizungumza na jarida la Maisha Rose alisema kuwa mchoro wa mchumba wake ni dhahiri kuwa ana mapenzi ya dhati kwani ni wanaume wachache wanaweza kufanya kitendo alichokifanya yeye na kutuma picha kama hiyo ambayo inaonekana na watu wengi
"Unajua mpaka mtu inafikia hatua ya kuweka wazi ni kwamba unajiamini na chaguo lako na pia kwa upande wangu inaonyesha kunijali na kunilinda na baadhi ya magonjwa maambukizi kwa kutojihusisha na mwanamke mwingine," alisem Rose
Pamoja na hayo alizungumzia juu ya harusi yake ambayo amesema kuwa muda ukifika ataweka wazi tarehe na mwezi wa siku yao ya kufunga ndoa
Picha hiyo ilionekana kuleta utata baada ya mchumba wake kuituma picha kwenye mitandao ya kijamii 'facebook' huku baadhi ya mashabiki wakituma maoni yao juu ya picha hiyo na kutaka kufahamu nini maana ya alama iliyokuwepo kwenye picha
TIMBULO WA "LEO WA KESHO" AINGIA BONGO MOVIE
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, rose ndauka 9:41 AM| Moja ya picha ya Timbulo na Rose Ndauka wakiwa location |
| -------------------------- |
Msanii wa bongo fleva Ally Timbulo maarufu kama Timbulo ivi sasa yuko katika michakato ya kufanya movi ambayo inaitwa "Ulimwengu wa faida" lakini pia katika movi hiyo wako mastaa wengine kibao kama Mzee Chiro, Hemed PHD huku Rose Ndauka pamoja na timbulo ndo watakua wahusika wakuu katika movi hiyo.
Msanii huyo ameamua kuingia katika bongo movi baada ya comenti nyingi sana kutoka kwa mashabiki wake kuwa anauwezo wa kufanya filamu kutokana na vipande ambavyo huwa anaigiza katika video zake za muziki.
Harakati za bongo.
Harakati za bongo.
ROSE NDAUKA UFUNGUKA KUHUSU SKENDO ZA UTAPELI ZINAZOMKABILI
Posted by Bigie habari za kitaifa, picha za utupu, rose ndauka 3:59 AMHabari mpya kutoka kwa Rose Ndauka baada ya kupiga story na mwandishi wa habari hii ni kuhusu skendo za utapeli.....
Mrembo huyu amefunguka na kusema kwamba kumekuwa na madai mengi sana kwamba amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii chipukizi na kuwachukulia fedha bila kuwashirikisha katika filamu zake.....
Ndauka alikanusha na kusema kwamba sio habari za kweli kwani anapoita usahili pale mtu anapofanya vizuri anamchukua na kama akifanya vibaya basi anamuelekeza ili siku nyingine atakapoitaji tena aweze kushiriki tena.
Hayo ndiyo maneno ya Rose Ndauka baada ya kuchonga nasi kuhusiana na tetesi ambazo zilikuwa zikizungumziwa kwamba anawachukia wasanii chipukizi wa filamu.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...




