ALBAM YA "MIDA YA KAZI" YA DULLAYO IPO MBIONI KUZINDULIWA


Msanii  nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abrahaman Kasembe ‘Dulayo’ ameachia videoni wimbo wake mpya wa Mida ya Kazi ambao umeanza kufanya vizuri katika stesheni mbalimbali za Televisheni.

Dulayo alisema kuwa video hiyo inakamilisha idadi ya video tatu alizitoa ambazo pia zinaendelea kutikisa katika medani ya muziki huo.

“Nimeshaiachia video yangu ya Mida ya Kazi na inafanya vizuri sana ambapo kwa zimeshakamilika video tatu ikiwa ni pamoja na Twende na Mimi na Naumia Roho” alisema.

Msanii huyo alisema kuwa ameshaanza maandalizi ya kuzindua albamu yake mpya ambayo itakwenda kwa jina la Mida ya Kazi ambapo nyimbo zote zimeshakamilika.

“Ninatarajia kuachia albamu ya Mida ya Kazi ambayo itakuwa na nyimbo 12 ambazo kwa sasa zimeshakamilika zote na ninamalizia mambo madogo madogo” alisema.

Anatarajia kufanya uzinduzi siku za usoni. Alisema baada ya uzinduzi huo, atazungunguka mikoa yote ya Tanzania kwa ya kufanya uzinduzi mikoani na baadaye Afrika Mashariki nzima ambapo uzinduzi pamoja na usambazaji utasimamiwa na Kampuni ya Sean Entertainment.

“Uzinduzi albamu yangu utakuwa tofauti zaidi kwani baada ya kuzindua Dar es Salaam itafuata mikoa yote ya Tanzania na baadaye Afrika Mashariki hiyo yote ni kwa ajili ya kuutangaza muziki wa bongo fleva katika nyanja mbalimbali.” Alisema Dullayo.
Alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zitakuwepo katika albamu yake kuwa ni pamoja na Naumia Roho, Twende na Mimi”,“Superstar”, “Mida ya Kazi”,Wa Ukweli” aliyomshirikisha Mr Blue, “Nimeamua”, “Chuzi Doa” aliyoimba na D.Knob, Kampani”, “Umepatwa na Nini”, “Bluetooth On”, “Valentine’s Day”, na “Muongo”.

HII NDO VIDEO YA WIMBO WA "MIDA YA KAZI"


Posted by Bigie on 8:19 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.