NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini


Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja  na Mara.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisini kwake Dr. Sisti  Kariah amesema kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha uandikishaji kwa BVR  katika mikoa  ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mara zoezi ambalo lilitarajiwa kuanza leo na  badala yake zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 16/06/2015.
 
Uamuzi wa kusogeza  mbele   unafuatia mabadiliko  ambayo yanaendelea kufanywa na Mipaka ya kiutawala ya kata, Vijiji, Vitongoji na Mitaa.
 
Uandikishaji kwa kutumia mfumo wa BVR unatoa fulsa kwa wananchi wote wenye  sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za Mpiga watatakiwa kujiandikisha upya. 
 
Zoezi la Uboeshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga hivisasa limefikia asilimia 50 kwa maana ya mikoa iliyofikiwa  na zoezi hilo nchini Tanzania.

Posted by Bigie on 5:37 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.