AUDIO: COLOUR KWA FACE BY NONINI FEATURING CHRISTINE APONDI



Siku chache zilizopita nilipokea taarifa kutoka kwa Msanii Nonini kutoka nchini Kenya kwamba ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Colour kwa Face kutoka katika album yake ya tatu aliyoipa jina The Godfather of Genge(ipo sokoni hivi sasa) akimshirikisha mwanadada Christine Apondi.


Kwa bahati mbaya sikupata muda wa chapchap wa kuusikiliza wimbo huu mpaka hivi leo.Katika wimbo huu Nonini ambaye ni mwanaharakati wa kutetea watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)anatuma ujumbe mpana sana kupitia wimbo huu.Kama mtakumbuka,Taifa letu la Tanzania liliingiwa na kashfa ya kimataifa pale ulimwengu ulipogundua kwamba kuna binadamu fulani wenye roho za ajabu wanawageuza watu wenye ulemavu wa ngozi “deal”.Nonini anaongelea hilo pamoja na mambo mengine ya kubaguana.Anaasa kupendana.Mpende kaka yako,mpende jirani na mpende kila mtu.Kwanini kubaguana?


Wimbo umetengenezwa na Musyoka kutoka Decimal Records.Usikilize…

Posted by Bigie on 5:30 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.