MASONGANGE ANUSURIKA KUFA

Mrembo anayedatisha katika video za nyimbo mbalimbali za Kibongo na mcheza filamu anayekuja kwa kasi, Agnes Gerald ‘Masogange’ ameponea chupuchupu kufa kwenye ajali mbaya ya gari na sasa hatamaniki midomo

Tukio hilo la kumpa pole, lilitokea wiki iliyopita, maeneo ya Sinza Kwaremmy jijini Dar es Salaam.

Masogange ambaye hivi karibuni ameanza kujipenyeza kwenye  filamu, alikutwa na ajali hiyo  akiwa ndani ya taksi akitokea nyumbani kwake Sinza Makaburini kwenda Kwaremmy kwenye mgahawa wa chakula wa Fast Food kutafuta mlo wa jioni.

Msanii huyo alisema kuwa ni wakati gari hilo likiwa linatafuta maegesho nje ya mgahawa huo ghafla  lilitokea gari lingine lililokuwa katika mwendo wa kasi na kuligonga gari alilokuwemo.

Alisema alipata mshtuko na msukumo mkubwa  uliomfanya ajigonge midomo kwenye kioo na kupasuka.

Aliongeza kwamba, mbaya zaidi baada ya ajali hiyo watu walilizunguka taksi wakiwemo vibaka ambao walitumia mwanya wa ajali  kumkwapulia  simu yake ya mkononi na fedha alizokuwa nazo (hakutaja kiasi).

 “Baada ya  kupata mzinga mimi nilijigonga kwenye kioo cha mbele cha gari  na kupasuka midomo. Baada ya hapo vibaka waliniibia simu na fedha, wakatimka,” alisema Masogange.
Hata hivyo,  Masogange alisema wasamaria wema walimchukua na kumpeleka  Kituo cha Afya cha Serikali Palestina, Sinza ambako alishonwa nyuzi tano.

 Akasema kwa taabu: “kikubwa kwa sasa namshukuru  Mungu kwa kuwa ilikuwa ajali mbaya ambayo ingeweza kukatisha maisha yangu.”

Posted by Bigie on 11:38 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.