MTUMISHI WA WIZARA YA ELIMU ANASWA AKIWA GESTI NA MUME WA MTU
JAMII 3:18 PM
Tukio hilo la kuchafua sifa ya ndoa, lilijiri hivi karibuni mjini Morogoro ambako Rose(mke wa Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ) aliaga kwa mumewe anakwenda kikazi.
Kapu la habari lililosheheni picha za video liliwasilishwa mbele ya gazeti moja maarufu hapa nchini hivi karibuni na mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sarah huku maelezo yakimtuhumu Rose kujivinjari na mumewe katika faragha haramu.
Habari zilieleza kwamba, mtumishi huyo wa wizara alidaiwa kuingilia ndoa ya mtu kwa kutumia safari zake za kikazi kula nyama ya ulimi na mume wa mtu huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kesi ambaye hatimaye alinaswa naye.
“Kuna watu waliniambia kuwa, Kesi ambaye ni mume wangu anatembea na mwanamke huyo, nikaanza kufuatilia hatua kwa hatua kwa kuwatumia watu wakiwemo watumishi wa hoteli aliyofikia Rose na mume wangu.
“Sikupenda kuwaingilia chumbani na kuwaharibia starehe zao, nilichotaka mimi ni ushahidi, nilitumia ujanja wangu kupenyeza kamera nikapata picha,” alisema Sarah huku akifungua kompyuta mpakato yake (laptop) na kuonesha tukio zima mbele ya ofisi ya gazeti hilo.
Katika kulithibitisha tukio,mtumishi huyu wa Wizara ya Elimu alipigiwa simu na maongezi yakawa kama ifuatavyo
Mwandishi: Habari yako dada Rose?
Rose: Nzuri, naongea na nani?
Mwandishi: Naitwa (tunalihifadhi) ni mwandishi wa Gazeti la Ijumaa.
Rose: Ndiyo, unasemaje?
Mwandishi: Aaa, hapa kuna tuhuma zako kwamba unatembea na mume wa mtu na kwamba hivi karibuni ulikuwa naye ndani ya gesti moja mjini Morogoro, lakini pia zipo picha za video na mnato zikionesha mambo machafu mliyoyafanya huko, sijui unajua chochote kuhusu hili?
Rose: We uko wapi, …kama ni ofisini nakuja sasa hivi kuziona hizo picha, nitakujibu nikifika.
Bila kuchelewa, dakika 27 baadaye Rose alifika katika ofisi za Ijumaa akiwa na mumewe na waliomba kuziona picha, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu wahariri kukubali zoezi hilo lifanyike mbele ya mwanaume huyo.
“Sikiliza kijana, huyu ni mke wangu, sasa unataka kuficha nini, umempigia simu, kaniambia, sisi tukakubaliana tuje wote kama mwili mmoja, sasa wewe unakataa nini…au ulikuwa na mambo yako?” alihoji kwa ukali mume wa mwanamke huyo.
Wahariri hatimaye walikubaliana na ombi la wanandoa hao kuona picha hizo kwa pamoja, hivyo walipelekwa kwenye kompyuta na kuanza kufunguliwa kifurushi kimoja baada ya kingine .
“Mume wangu tulikuwa tumekaa tu hapa, huyu kaka alikuja kunitembelea chumbani, umeona nimevua nguo?” Rose alijitetea kwa mumewe baada ya kifurushi cha kwanza kufunguliwa na kuwaonesha wakiwa wamekaa kitandani na jamaa.
Hata hivyo, mwanamke huyo alibadilisha maelezo baada ya kufunguliwa video ya pili iliyowaonesha wakiwa katika ‘kikilikakala’ za watu wazima walizokuwa wakifanya gesti siku hiyo ambapo Rose alijikuta akisema: “Mume wangu huyu kaka alinilazimisha mimi nilikuwa sitaki kabisa.”
Kauli hiyo ya mtumishi huyo wa umma mbele ya mumewe ilikuwa kama kutia nazi kwenye supu kwani kimsingi video iliwaonesha wawili hao wakishirikiana ipasavyo hali iliyomfanya mumewe ashushe pumzi.
Mpaka mwisho wa sinema hiyo yenye dakika chache lakini zenye ‘machungu’, wanandoa hao waliondoka wakiwa ‘wamelowa’ jasho
HABARI HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA MAGAZETI PENDWA YA GLOBAL PUBLISHER .JIPATIE NAKALA YAKO LEO
SKENDO NYINGINE:
MHESHIMIWA SPIKA AFUMANIWA GEST AKIVUNJA AMRI YA SITA NA MWANAFUNZI








