NAIBU WAZIRI WA ELIMU MH.PHILIP MULLUGO ATOA MSAADA WA LAPTOP 40, VITABU 6000, NA MADAWATI 80 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA JIMBO LA SONGWE
JAMII 10:25 PM
Naibu Waziri wa elimu na mbunge wa jimbo la Songwe mkoani Mbeya Philip Mullugo ametoa vitabu 6,000 vya Sekondari na Msingi, Compyuta 40 (Laptop) kwa walimu, Madawati 80 ya kisasa ya katika Sekondari za kata wilayani Chunya.
Akizungumza na mwandishi wetu Naibu Waziri Mullugo amesema kuwa ametoa vifaa hivyo ili kuiwezesha wilaya hiyo kuendelea kielimu.
Aidha ameahidi kutoa shilingi milioni 70 kwa ajili ya kuchimba visima 17 vitakavyosaidia kupunguza tatizo la maji wilayani humo hasa kwa shule za sekondari za kata.





