50 CENT YUPO MBIONI KUTOA MKANDA WA KIVITA UITWAO "THE PURSUIT" --HILI NI SIMULIZI FUPI LA MKANDA HUU

  
   50 cent yupo mbioni kukamilisha mkanda wake wa kivita uitwao   "THE PURSUIT"   kupitia kampuni yake iitwayo "Cheetah Vision Films"
 
      Mkanda huu wa kivita unaoongozwa na mwongozaji mahiri   "Jessy Terrero"  unahusu harakati za komamdoo  50 cent  ambaye anaungana na askari kadhaa kumsaka mtu mmoja aliekuwa amevamia benki moja maarafu nchini Marekani kwa lengo la kulipiza kisasi

    .Jambazi hilo liliiteka benki hiyo na kusababisha uhalibifu mkubwa.Katika harakati za kulisaka jambazi hili,damu nyingi isiyo na hatia inamwagika,na hivyo kuulazimisha mtandao wa Marshall kuingilia kati ili kuzuia huu umwagaji wa damu na pia kuhakikisha kuwa Jambazi hili linatiwa nguvuni haraka iwezekenavyo

     Akielezea katika hatua za awali za mkanda huu,Producer alisema kuwa  tayari FIDDY  amesha saini na kukubali kuwa ataigiza kama "askari" (cop).Aliongeza kwa kusema kuwa,mkanda huu wa kivita unategemewa  kutoka mwezi wa pili mwakani (2012)


 

Posted by Bigie on 7:48 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.