BASI LA LINDI LAJERUHI WATU 35
JAMII 2:03 AM


Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la Ng'itu lenye No.T804 BAF wamenusurika kifo baada ya gari lao kupata ajali katika kijiji cha Sinza - Miteja katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Katika ajali hiyo watu 35 wamejeruhiwa vibaya na kuwahishwa kwenye hospital jirani kwa matibabu. Ajali hiyo imeshuhudiwa na watu wengi wakiwemo wakuu wa Mikoa ya Dar es salaam na Mkuu mpya wa Mkoa wa Lindi ambao walikuwa katika Makabidhiano ya Mkoa huo.






