FAMILY DAY ILIVYOKUWA NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS CLUB
JAMII 3:31 PM
Shabiki akilicheza goma la Prakatatumba vilivyo jukwaani.
Meneja wa Cabo snoop akimchemsha kidogo Dj,aachie ngoma ya Windeck watu waserebuke pamoja na msanii Cabo Snoop.
Wakali wa Chakachaka walikuwepo pia kunogesha bonanza hilo
Pamoja na kuwepo na hali ya mvua mvua kiaina.lakini watazamaji wala hawakukata tamaa,badala yake viti viliwekwa kichwani kuzuia mvua,mambo yakaendelea jukwaani kama kawa.
Wasbaiki kutoka kona mbalimbali ya jiji la Dar walijitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Family Day,jioni ya leo ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Palikuwa hapatoshi na songi la Prakatatumba kutoka kwa Cabo Snoop,pichani huku akichagizwa na Meneja wake.
Msanii mdogo lakini mambo yake makubwa,ambaye anatamba na wimbo wake wa "NAENDA KUSEMA",anaitwa Islay ikitumbuiza mbele ya umati wa watu waliofika kwenye Family Day Bonanza,lililofanyika Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Wakazi wa jiji la Dar wakiwa wamejitokeza kwa wingi leo mchana kwenye bonanza la Family Day lililoandaliwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions/Clouds Media Group
Watoto wakiserebuka kivyao .
Ni siku ya family day ndani ya viwanja vya Lidaz Club,wengi wamejitokeza pia kuburudishwa na burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa viwanjani hapo,ikiwemo na kumshuhudia mwanamuziki wa kimataifa kutoka nchini Angola,Cabo Snoop.
Watoto walichorwa kama hivi.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions,pichani kati aliyevaa miwani,Juhayna Kusaga akiwa na baadhi ya marafiki zake pamoja na watoto wao kwa pamoja wakisherehekea Family Day ndani ya viwanja vya Lidaz Club,jijini Dar.
Palinoga Lidaz Club.
Densas wa bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza jukwaani .
Watazamaji wakiendelea kufuatilia yanayojiri jukwaani



















